Kiendeshi diski kuu
Kutoka Wikipedia
Diski kuu au kiendeshi diski kuu ni sehemu ya kompyuta ambako kumbukumbu ya habari hutunzwa. Inaitwa pia kwa kifupi chake cha Kiingereza HDD (hard disk drive) au HD (hard drive). Inaitwa diski kuu kwa sababu komputa hutumia diski mbalimbali kwa mfano CD au diski ndogo aina ya flopi.
Yaliyomo |
[hariri] Muundo wa HDD
Diski kuu kwa kawaida inaonekana kama sanduku ndogo ya metali iliyofungwa kabisa. Ndani yake kuna diski inatunza kumbukumbu ya habari yote yaliyowekwa mle. Sanduku imefungwa kabisa ili vumbi au takataka isiingie ndani.
Ndani ya sanduku ya nje kuna diski nyembamba au visahani moja, mbili au zaidi. Zinatengenezwa kwa kioo au aloi ya alumini. Diski hii imefunikwa kwa ganda la aloi lenye tabia ya kisumaku.
[hariri] Kazi ya HDD
[hariri] Kuandika
Diski inazungushwa kwa injini ya uememe ndogo haraka sana hadi mara 15,000 kwa dakika. Mkono unaoshika kalamu sumaku (huitwa pia "head" - kichwa) unapita juu yake. Kalamu unaacha alama sumaku kwenye mahali padogo usoni wa diski. Mfululizo wa nukta yenye chaji na nukta bila chaji inatunza habari kwa mfano herufi za alafabeti au pia picha. Chaji inabaki mahali pake kutokana na sifa za aloi inayofunika diski.
[hariri] Kusoma
Wakati wa kusoma habari mkono unapita juu ya uso wa diski na kalamu inafanya kazi kinyume ya kuandika safari hii inagundua alama sumaku zilizopo na mfululizo wa nukta sumaku na nukta bila alama ya sumaku unasomwa na tarakilishi.
[hariri] Kufuta
Wakati wa kufuta kumbukumbu mkono unapita juu ya sehemu ya diski ambako habari inatakiwa kufutwa na kuondoa chaji.
Kuna hatari ya kuweka sumaku karibu na kompyuta kwa sababu sumaku inaweza kuathiri kumbukumbu kwenye diski.
[hariri] Kuongezeka kwa nafasi ya kutunza habari
Alama za sumaku hubaki kwenye diski kwa miaka mingi kama haiandikwi upya. Mabadiliko ya teknolojia yameongeza uezo wa kutunza habari kila baada ya miaka kadhaa. Nafasi ya kumbukumbu hupimwa kwa baiti na baiti moja ni kiasi cha alama sumaku zinazoeleza herufi moja. "Neno" lina herufi nnne hivyo inahitaji nafasi ya baiti nne kwenye diski. Baiti milioni 1 inaitwa megabaiti; megabaiti milioni huitwa gigabaiti. Kompyuta za miaka mnamo 1985 zilishika kiasi cha habari cha megabiti 20-40. Mnamo 1992 diski za megabaiti 400 zilkikuwa kawaida. Tangu 1995 diski zenye gigabaiti zimepatikana, na 2005 diski ya gigabaiti 500 ilipatikana. Tayari terabaiti (milioni gigabaiti) ieanza kupatikana kwenye diski kuu mpya tangu 2007-08.
Maana yake ni ya kwamba kiasi cha habari kinachotunzwa kwenye kompyuta moja imeongezeka mfululizo. Awali kompyuta iliweza kushika maandishi ya kitabu kidogo; baadaye vitabu kadhaa halafu maktaba. Diski kubwa za siku hizi zinatafutwa kwa sababu watu wameanza kunakili filamu kwenye tarakilishi zao.
[hariri] Wakati ujao
Kuna malalamiko juu ya diski kuu kwa sababu matumizi yake ya umeme pamoja na sauti inayotoa yamesumbua watu. Kompyuta ndogo zaidi zisizohitaji kutunza kiasi kikubwa sana cha data hutumia tayari vifaa vya kumbukumbu ya flash visivyohitaji injini hivyo haviharibiki haraka kama vile diski kuu.