Borneo
Kutoka Wikipedia
Borneo ni kisiwa kikubwa cha pili cha Asia ya kusini-mashariki. Eneo lake ni 740,000 km². Duniani visiwa vya Greenland na Guinea Mpya pekee ni vikubwa zaidi.
Borneo hutawaliwa na nchi tatu:
- Sehemu kubwa katika kusini iko chini ya Indonesia inaitwa Kalimantan.
- Kaskazini ni eneo la Malaysia ya Mashariki au majimbo yake ya Sarawak na Sabah.
- Ndani ya eneo la Malaysia iko usultani mdogo wa Brunei.
Hali ya hewa ni ya kitropiki. Maeneo makubwa ni misitu minene.
Idadi ya wakazi ni milioni 15.7 (2005) na msongamano wa watu ni wakazi 16/km².
Watu ni Wadayak, Wamalay na Wachina.
Makala hiyo kuhusu "Borneo" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Borneo kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |