Asenia
Kutoka Wikipedia
Asenia (arseniki) |
|
---|---|
|
|
Jina la Elementi | Asenia (arseniki) |
Alama | As |
Namba atomia | 33 |
Mfululizo safu | Simetali |
Uzani atomia | 74.9216 |
Valensi | 2, 8, 18, 5 |
Densiti | 1.9 hadi 5.72 kufuatana na alotropia zake |
Kiwango cha kuyeyuka | 1090 K (817 ° °C) |
Kiwango cha kuchemka | 887 K (614°C) (mvukemango) |
Asilimia za ganda la dunia | 6 · 10-4 % |
Hali maada | mango |
Mengineyo | Asenia ni tahajia ya KAST, Aseniki ya ILSD, Arseniki penginepo katika mtandao |
Asenia (pia: arseniki, aseniki; kutoka kigiriki αρσενικόν "arsenikon" iliyotaja kampaundi ya elementi) ni nusumetali au metaloidi yenye namba atomia 33 katika mfumo radidia. Uzani atomia ni 74.9216.
[hariri] Tabia
Asenia ina tabia ya alotropia kwa hiyo kuna maumbo na rangi mbalimbali. Kuna hasa maumbo yenye rangi za kijivu, nyeusi, njano na kahawia. Asenia ya kijivu ina fuwele na tabia za kimetali. Asenia nyeusi hupatikana kwa umbo hobela kama kioo.
Asenia ni sumu kali kwa binadamu.
[hariri] Matumizi
Kampaundi za asenia hutumiwa kama madawa katika tiba ya watu lakini pia madawa ya kuua wadudu. Madawa yaliwahu kuleta hasara ya kiafya hata kuua watu.
- Mwaka 1900 walikufa watu 70 mjini Manchester (Uingereza) kwa sababu kiwanja cha bia kilitumia nafaka iliyowahi kutiwa madawa ya asenia kwa kuua wadudu.
- katika karne ya 20 bao za ujenzi zitiliwa mara nyingi dawa la asenia kwa kuzuia wadudu. Bao hazikuwa na hasara lakini imeonekana baadaye ya kwamba majivu ya ubao huu kama ulichomwa motoni yalikuwa hatari sana; gramu 20 za majivu ya ubao huo zikatosha kumwua mtu; maafa yalitokea baada ya watoto kuecheza kwenye majivu au wanyama kulamba maji karibu na mahali pa moto baada ya mvua.
Asenia ikichanganywa na risasi (metali) (plumbi) husaidia katika kutengenezwa kwa beteri za gari ikiboresha umwagaji wa plumbi kiwandani.
Makala hiyo kuhusu "Asenia" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Asenia kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |