Antigua na Barbuda
Kutoka Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Each Endeavouring, All Achieving (Jaribu kila kitu, Faulu kila kitu) | |||||
Wimbo wa taifa: Fair Antigua, We Salute Thee (Antigua mzuri twakusalimu) Wimbo la kifalme: God Save the Queen1 |
|||||
Mji mkuu | Saint John's |
||||
Mji mkubwa nchini | Saint John's | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza | ||||
Serikali | Ufalme wa Kikatiba Elizabeth II wa Uingereza Sir James Carlisle Baldwin Spencer |
||||
Uhuru kutoka Uingereza |
1 Novemba 1981 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
442 km² (ya 198) -- |
||||
Idadi ya watu - 2005 kadirio - Msongamano wa watu |
81,479 (ya 197) 184/km² (57) |
||||
Fedha | East Caribbean dollar (XCD ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
AST (UTC-4) ADT (UTC-3) |
||||
Intaneti TLD | .ag | ||||
Kodi ya simu | +268 |
||||
1 God Save The Queen ni kama wimbo la taifa lakini hutumiwa tu kwenye nafasi za kifalme. |
Antigua na Barbuda ni nchi ya visiwani ya Amerika ya Kati kwenye bahari ya Karibi. Kuna visiwa viwili vya Antigua na Barbuda vinavyokaliwa na watu pamoja na kisiwa kidogo cha Redonda kisicho na wakazi.
Antigua na Barbuda ni sehemu ya funguvisiwa vya Antili Ndogo pamoja na Guadeloupe, Dominica, Martinique, Saint Lucia, Saint Vincent na Grenadini, Barbados, Grenada, Trinidad na Tobago upande wa kusini halafu Montserrat, Saint Kitts na Nevis, Saint Barthélemy, Saint Martin na Anguilla upande wa magharibi.
Idadi ya wakazi ni watu 69,108. Wengi wao hukaa Antigua. Barbuda ina watu 1,500 pekee. Walio wengi sana (zaidi ya 90 %) wametokana na watumwa Waafrika waliopelekwa hapa wakati wa ukoloni.
Nchi hufuata utaratibu wa ufalme wa Uingereza. Ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Madola. Mkuu wa dola ni malkia Elizabeth II wa Uingereza anawakilishwa na Gavana Mkuu. Serikali iko mkononi mwa waziri mkuu anayetegemea kura za bunge.