Adria
Kutoka Wikipedia
Bahari ya Adria au kwa kifupi "Adria" ni ghuba ya Mediteranea kati ya Rasi ya Italia na Rasi ya Balkani. i
Nchi zinazopakana nayo ni Italia, Slovenia, Kroatia, Bosnia na Herzegovina, Montenegro na Albania.
Adria huelekea kaskazini magharibi kutoka 40°N hadi 45° 45' N.. Urefu wake ni km 770 km na upana waka kwa wastani ni km 160. Sehemu nyembamba ni mlango wa Ortranto mwenye upana wa km 85. Eeno lake ni mnamo km² 160,000.
Mwambao wa kaskazini una visiwa vingi hasa mbele ya pwani la Kroatia.