Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Witu - Wikipedia

Witu

Kutoka Wikipedia

Witu ni mji mdogo na tarafa katika Mkoa wa Pwani, wilaya ya Lamu nchini Kenya. Iko barabarani kutoka Malindi kwenda Lamu, takriban katikati ya mto Tana na Lamu.

[hariri] Historia

Historia ya Witu ilianza mwaka 1858 BK. Sultani wa Pate Ahmad ibn Fumo Bakari aliyezaliwa katika familia ya watawala wa Nabahani alijenga makao mapya barani kwa sababu alitaka kujiokoa na Usultani wa Zanzibar uliotafuta utawala juu ya funguvisiwa ya Lamu wakati ule.

Mashambulio ya Wazanzibari yaliendelea na kumsababisha sultani kuomba msaada wa ulinzi wa Ujerumani mara ya kwanza mwaka 1867. Mwaka 1885 Sultani alifunga mkataba na ndugu Wajerumani Clemens na Gustav Denhardt akaweka nchi yake chini ya ulinzi wa Dola la Ujerumani kuanzia tar. 27.05. 1885. Kama shukrani kwa ndugu Denhardt aliwapa eneo la maili za mraba 25 akawafanya kuwa mawaziri yake.

Sultani wa Zanzibar hakufurahia habari hizi wala mbalozi wa Uingereza Zanzibar mjini. Lakini mipango yao dhidi ya Witu ilishindikana kwa sababu serikali ya Ujerumani ilituma manowari SMS Gneisenau Afrika ya Mashariki na wanajeshi 30 Wajerumani walipiga kambi Witu. 1888 Ujerumani ilifungua ofisi ya posta Lamu mjini kwa ajili ya mawasiliano kati ya Witu na Ujerumani kwa sababu meli zilipita mara kwa mara Lamu ilhali Witu haikuwa na bandari kamili.

Serikali ya Ujerumani haikuonyesha nia ya kuimarisha utawala wake kwenye pwani la Kenya; iliona Witu kama bidhaa kwa ajili ya biashara na Waingereza. Katika mkataba wa Helgoland-Zanzibar Witu iliachiliwa Uingereza na ulinzi wa Ujerumani ulikwisha 01. 07. 1890.

Wenyeji wa Witu hawakupendezwa na mabadiliko haya kwa sababu waliogopa ya kwamba watafikishwa chini ya Zanzibar angalau waliwajua Waaingereza kuwa karibu sana na Sultani wa Zanzibar. Walisikia kuwa Wajerumani waliwasaliti. Katika September 1890 ilitokea ugomvi mkali. Mfanyabiashara Mjerumani Andreas Küntzel alitegemea kuanzisha biashara katika eneo la Sultani lakini alikataliwa kwa sababu ya hasira iliyosababishwa na mkataba wa Julai 1890. Wenzake Küntzel walijaribu kulazimisha maafisa wa Sultani kwa kuonyesha silaha lakini walikamatwa na silaha zao kuchukuliwa. Küntzel alijaribu kuwaweka huru akamtukana sultani mbele ya watu wake. Wenyeji wenye hasira waliwaua Wajerumani wale na kushambulia Wazungu wengine. Jumla Wajerumani 9 waliuawa wengine wakakimbia.

Waingereza walituma jeshi chini ya Admirali Sir E. Freemantle wakavamia Witu katika Septemba 1890. Tar 28.10.1890 Mji Mkuu wa Witu ulichomwa moto na Waingereza. Lakini mapigano yaliendelea Kuna makadirio ya kwamba wenyeji 500 waliuawa, mji Witu ikaharibika na Sultani alitupwa jela alikokufa. Mapigano yaliendelea hadi 1894 Witu ikawa koloni ya Uingereza. Katika mkataba wa Helgoland-Zanzibar Uingereza iliahidi ya kwamba itaheshimu mipaka ya eneo la Witu. Awali Waingereza walimteua sultani mpya Omar-bin-Hamed aliyetoka katika ukoo wa Nabahani vilevile.

Lakini baadaye hawakuheshimu tena usultani wa Witu jinsi walivyowahi kuahidi katika mkataba wa 1890 wakaitendea kama sehemu ya mkoa wa Tana tu.

Baada ya kifo cha Sultani mwaka 1923 usultani ulikwisha kabisa.

[hariri] Viungo vya nje


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -