Sua
Kutoka Wikipedia
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kipo katika manisipaa ya Morogoro nchini Tanzania. Hiki ni chuo kikuu pekee cha kilimo nchini. Lilipewa jina kwa heshima ya mwanasiasa marehemu Edward Sokoine.
Chuo hiki kilianzishwa mwaka 1984 na kabla ya hapo kilikuwa ni chuo kikuu kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tangu mwaka 1970.
Mwaka 1984 chuo hiki kilianza na vitivo vitatu:
- kitivo cha kilimo
- kitivo cha misitu pamoja na
- kitivo cha tiba za mifugo
na hivi karibuni kimeanzishwa
- kitivo cha sayansi.
Chuo kinadahili wanafunzi wa shahada za kwanza na za uzamili katika vitivo vyote isipokuwa kitivo cha sayansi ambacho hakitowi shahada za uzamili. Chuo kina wanataaluma zaidi ya mia tatu na kwa mwaka huu wa masomo kimedahili wanafunzi wa shahada za kwanza wapatao 2400 na wale wa shahada za juu zaidi ya mia mbili.
SUA ina chuo kishiriki cha MUCCoBS (Moshi University College Of Cooperatives and Business Studies) katika mkoa wa Kilimanjaro.