Snorri Sturluson
Kutoka Wikipedia
Snorri Sturluson (Kiiceland Snorri mwana wa Sturluson, * 1178; † 22 Septemba 1241) alikuwa mshairi, mwandishi wa historia na kiongozi wa kisiasa nchini Iceland.
Anajulikana hasa kama mtungaji wa kitabu cha Edda kinachokusanya habari za utamaduni na dini ya Iceland ya kale kabla ya kufika kwa Ukristo pamoja na kanuni kwa kazi ya mshairi na mwimbaji wa shairi zinazosimulia historia ya taifa. Aliandika üpia historia ya wafalme wa Norway.
Mwenyewe alipokea mafunzo ya kuandika na kusoma, pia lugha ya Kilatini, elimu ya dini ya Kikristo na sheria ya Kiiceland. Wazazi walimkabidhi kwa chifu mkubwa aliyemlea kijana.
Alichaguliwa baadaye mara mbili kama msimamizi wa Althing iliyokuwa bunge la Iceland.