Sinai (mlima)
Kutoka Wikipedia
Mlima Sinai (Kiar.: جبل موسى jabal musa = mlima wa Musa) ni mlima mwenye kimo cha 2,283 m juu ya UB katika kusini ya Rasi ya Sinai nchini Misri. Inajulikana kama kwa majina ya Mlima wa Horeb au kwa jina lake la Kiarabu kama Gebel Musa (matamshi ya Kimisri) au Jabal Musa (matamshi ya Kiarabu sanifu).
Mlima Sinai unaaminiwa tangu kale kuwa ni mahali ambako Musa alipokea amri kumi kutoka Mungu wakati wa kutoka kwa Wanaisraeli katika utumwa wa Misri.
Kilele cha mlima kina kanisa la Kiorthodoksi lenye asili ya jengo la Kaisari Justiniano I la mwaka 532 na pia msikiti ya karne ya 12. Monasteri ya Mt. Katarina iko kwenye mwanzo wa mlima.