Sao Tome
Kutoka Wikipedia
Sao Tome ni mji mkuu wa nchi ya visiwa ya Afrika ya Magharibi ya Sao Tome na Principe. Jina limetokana na Kireno cha Mtakatifu Thomas.
Mji umeanzishwa na Ureno mwaka 1485 ukiwa kwenye pwani la kaskazini-mashariki la kisiwa chenye jina lilelile katika ghuba ya Guinea.
Mji ulikuwa na wakazi 53,300 mwaka 2004. Kuna kiwanja cha ndege cha kimataifa na viwanda kadhaa ya matofari, sabuni na vinywaji. Sao Tome ina shule za msingi hadi sekondari, makanisa, hospitali ya pekee nchini, vituo vya TV na redio.