Samos
Kutoka Wikipedia
Samos ni kisiwa cha Ugiriki kilichopo kilomita 1.3 mbele ya pwani la Uturuki. Ni pia moja ya wilaya 51 za Ugiriki.
Samos ina urefu wa 44 km na upana wa 19 km, eneo lake ni 477 km². Sehemu kubwa ni milima inayofikia kimo cha 1,153 m.
Kuna wakazi 33,800 na mji mkubwa unaitwa Samos vilevile ina watu 6,000. Uchumi unategemea utalii pamoja na kilimo. Divai ya Samos ni maarufu.
Katika historia ya Ugiriki ya Kale Samos ilikuwa nyumbani kwa wataalamu mashuhuri kama Pythagoras, Epikuri na Herodoti.
Makala hiyo kuhusu "Samos" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Samos kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |