Ndege-mawingu
Kutoka Wikipedia
Ndege-mawingu | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Ndege-mawingu mkia-mweupe
|
||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Ndege-mawingu ni ndege wa bahari katika jenasi Phaethon, jenasi pekee ya familia Phaethontidae. Ndege hawa ni weupe na wana mileli mirefu katikati ya mkia. Hupitisha maisha yao yote baharini isipokuwa wakati wa majira ya kuzaa. Wanaweza kuogelea na kwa hivyo wana ngozi kati ya vidole; kwa kweli hawatembei vizuri. Huwakamata samaki na ngisi wakipiga mbizi au huwakamata panzi-bahari (samaki wanaoruka juu ya maji). Hutaga yai moja tu ndani ya tundu au mwanya wa mwamba visiwani kwa bahari.
[hariri] Spishi za Afrika
- Phaethon aethereus, Ndege-mawingu Domo-jekundu (Red-billed Tropicbird)
- Phaethon rubricauda, Ndege-mawingu Mkia-mwekundu (Red-tailed Tropicbird)
- Phaethon lepturus, Ndege-mwingu Mkia-mweupe (White-tailed Tropicbird)