Mwai Kibaki
Kutoka Wikipedia
Mwai Kibaki | |
---|---|
|
|
Rais wa tatu wa Kenya | |
Tarehe ya kuzaliwa | 15 Novemba 1931 |
Mahali pa kuzaliwa | kijiji cha Gatuyaini, tarafa ya Othaya, wilaya ya Nyeri |
Chama | hadi 1991 KANU, halafu DP, 2002 NARC |
Alingia ofisini | 2002 |
Alitanguliwa na | Daniel arap Moi |
Dini | Mkristo Mkatoliki |
Elimu yake | chuo kikuu cha Makerere, LSE London |
Digrii anazoshika | M.Sc. (Public Finance |
Kazi | mwalimu wa chuo, mwanasiasa |
Mwai Kibaki ni rais wa tatu wa Jamhuri ya Kenya akiwa ametanguliwa na Rais wa Kwanza wa Kenya,Mzee Jomo Kenyatta, na Daniel Arap Moi. Jina lake la kubatizwa ni Emilio Stanley .
Kibaki alisoma uchumi, historia na sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda. Akiwa mwanafunzi Makerere, Kibaki alikuwa ni mwenyekiti wa chama cha wanafunzi toka Kenya, Kenya Students' Association. Alipomaliza masomo yake mwaka 1955 alipewa tuzo kutokana na kufanya vyema katika mitihani. Tuzo hiyo ilimwezesha kwenda kusoma katika chuo cha London School of Economics. Alipomaliza masomo alikwenda kufundisha katika chuo kikuu cha Makerere. Baadaye aliacha kazi ya kufundisha na kuwa mtendaji mkuu wa chama cha Kenya African National Union.
Kibaki, licha ya kuwa mbunge, amewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwenyekiti wa Tume ya Mipango, Waziri wa Biashara na Viwanda, na Waziri wa Fedha. Moi alipoingia madarakani baada ya kifo cha Jomo Kenyatta, Kibaki aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais.
Mwaka 1988 Kibaki alianza kuwa na mgongano na Rais Moi. Mwaka huo alivuliwa Umakamu wa Rais na kupelekwa Wizara ya Afya.
Mwaka 1991 Kibaki aliondoka chama cha KANU na kuanzisha chama cha Democratic Party. Katika uchaguzi wa Urais wa mwaka 1991, Kibaki alikuwa wa tatu na mwaka 1997 alikuwa wa pili.
Yaliyomo |
[hariri] Uchaguzi wa urais 2002
Katika uchaguzi wa 2002 Kibaki alishinda na kutangazwa kuwa Rais wa Kenya. Alikuwa mgombea wa maungano wa vikundi vingi vya upinzani vilivyoshirikiana kwa jina la "NARC".
Kibaki ameweka historia mwezi Novemba, 2005 baada ya kuwa Rais wa kwanza nchini Kenya kuondoa baraza lote la mawaziri kufuatia kura ya maoni ambayo ilikuwa inahusu katiba mpya ya Kenya. Kibaki alikuwa upande wa kundi lililokuwa likiunga mkono katiba hiyo kambi ya ndizi. Kundi lililokuwa likiipinga katiba hiyo kambi ya machungwa lilipata ushindi.
[hariri] Uchaguzi wa urais 2007
Uchaguzi wa 28 Desemba 2007 ulimrudisha Kibaki kwa kipindi cha pili kama rais. Uchaguzi huu ulipingwa na chama cha upinzani na watazamaji wa kimatifa kuwa matokeo yake hayakuwa sahihi na kubiniwa. Mpinzani wake Raila Odinga alikuwa mbele katika hesabu za kura hadi kamati ya uchaguzi ilisimamisha hesabu ya kura; baada ya kuendelea na matanganzo Kibaki alionekana kuwa mbele. Kuna hofu ya kwamba matokeo ya majimbo ya uchaguzi kadhaa yalibadilishwa upande wake kwa kumwongezea kura. Kibaki aliapishwa upya kuwa rais wa Kenya masaa machache tu baada ya kutangazwa kuwa mshindi; hafla ilifanywa katika bustani ya ikulu ya Nairobi bila wananchi kuruhusiwa kushuhudia.
Kinyume cha uchaguzi wa rais uchaguzi wa Bunge la Kenya 2007 uliendelea bila matatizo makubwa.
[hariri] Serikali ya Januari 2007
Baada ya kutangazwa kuwa rais mpya Kibaki aliteua mawaziri 17 kama awamu ya kwanza ya serikali akiacha nafasi nyingine serikalini kando kwa muda.[1]
- (1) Makamu wa Rais na waziri wa mambo ya ndani: Stephen Kalonzo Musyoka
- (2) Waziri wa utawala wa mikoa na usalama wa ndani katika Ofisi ya Rais: George Saitoti
- (3) Waziri wa ulinzi katika Ofisi ya Rais: Yussuf Mohamed Haji
- (4) Waziri wa mipango maalumu katika Ofisi ya Rais: Dr. Naomi Namsi Shaban
- (5) Waziri wa utumishi wa serikali katika Ofisi ya Rais: Asman Abongotum Kamama
- (6) Waziri wa fedha: Amos Muhinga Kimunya
- (7) Waziri wa elimu: Sam Ongeri
- (8) Waziri wa mambo ya nje: Moses Wetangula
- (9) Waziri wa serikali ya mitaa: Uhuru Kenyatta
- (10) Waziri wa habari na mawasiliano: Samuel Lesuron Poghisio
- (11) Waziri wa maji na umwagiliaji: John Munyes
- (12) Waziri wa nishati: Kiraitu Murungi
- (13) Waziri wa barabara na kazi za umma : John Njoroge Michuki
- (14) Waziri wa sayansi na teknolojia: Noah M. Wekesa
- (15) Waziri wa sheria na mambo ya katiba: Martha Karua
- (16) Waziri wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki: Dr. Wilfred Machage
- (17) Waziri wa usafiri: Chirau Ali Mwakwere
[hariri] Viungo vya Nje
- ↑ http://www.eastandard.net/news/?id=1143980114 Kibaki names cabinet EA Standard 08-01-2008