Muharram (mwezi)
Kutoka Wikipedia
Muharram (Kiarabu: محرم ) ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kiislamu. Ni kati ya miezi minne mitakatifu ya mwaka. Jina la mwezi limetokana na neno "haram" yaani "mwiko" au "kukatazwa" kwa maana ya kwamba vita haitakiwi mwezi huu.
Siku ya kwanza wa Muharram ni Mwaka Mpya wa Kiislamu.
Sikukuu ya Ashurah iko mnamo tar. 10 Muharram. Hasa Waislamu Washia hukumbuka kifo cha khalifa Ali kwenye mapigano ya Kerbela.