Moshi (mji)
Kutoka Wikipedia
Moshi ni makao makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania.
Yaliyomo |
[hariri] Wakazi
Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002, mji huu una wakazi wapatao 144,739. Kabila linaloongoza kwa idadi ya wakazi wa mji wa Moshi ni Wachagga. Kuna makabila mengi kama Wapare, Wanyakyusa, Wasukuma, Warangi, Wasambaa n.k. Wachagga wanapenda vyakula vinavyopikwa kwa kutumia ndizi kama vile mtori, kitawa, na machalari.
Wakazi wengi wa Moshi ni wakulima, wafugaji na wafanyabiashara. Watu wengi wanaenda Moshi kufanya kazi na kurudi nyumbani jioni.
Ukuaji wa mji wa Moshi hauendani na mipango halisi ya 'Mipango Miji'. Hii inatokana na kutokufuatiliwa kwa sheria mbalimbali zinazohusu uendelezaji wa miji.
[hariri] Hali ya Hewa
Moshi ni mji wenye baridi katika miezi ya Juni mpaka Agosti na kipindi cha joto katika miezi ya Oktoba hadi katikati ya Januari.
[hariri] Utalii
Mji wa Moshi una mandhari nzuri ya kuvutia watalii. Watalii hupenda sana mji wa Moshi kwa sababu ya mlima Kilimanjaro na huduma muhimu kama mahoteli na usafiri.
[hariri] Elimu
Mji wa Moshi una vyuo vikuu vitatu:
- MUCCoBS (Moshi University College Of Cooperative and Business Studies) ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro
- MWUCE (Mwenge University College Of Education) ambacho ni chuo kikuu kishiriki cha SAUT (St. Augustine University - Mwanza)
- KCMC Medical School chini ya Chuo Kikuu cha Tumaini