Liwali
Kutoka Wikipedia
Kwa "wali" kama chakula tazama wali (chakula)
Liwali au wali ni cheo cha msimamizi wa eneo fulani.
Asili ni neno la Kiarabu "ولي" linalomaanisha mtawala wa mahali au eneo asiyejitegemea bali aliyeteuliwa na serikali kushughulikia mambo ya utawala katika eneo fulani. Mara nyingi katika nchi za utamaduni wa Uislamu Wali alisimamia "wilaya".
Katika eneo la Waswahili maneno ya wali au liwali yalichanganywa kwa maana moja kumtaja mkuu wa mahali au wa mji.