Kwale (ndege)
Kutoka Wikipedia
Kwale | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kwale shingo-njano
|
||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Kwale ni ndege wa jenasi Francolinus na Xenoperdix katika familia ya Phasianidae. Spishi nne za Francolinus ambazo zina ngozi kichele yenye rangi kali kooni na pande zote za macho huitwa kereng'ende pia. Rangi ya kwale ni kahawia au kijivu na wana michirizi au madoa. Mara nyingi miguu yao ni myekundu au rangi ya manjano na koo lao ni jekundu, jeupe, jeusi au rangi ya manjano. Hujificha kwa kawaida lakini sauti yao husikika mara kwa mara. Chakula chao ni mbegu, wadudu na nyungunyungu. Hutaga mayai matatu hadi kumi ardhini pengine juu ya manyasi makavu.
Karibu spishi zote zinatokea Afrika lakini spishi tano zinatokea Asia.
[hariri] Spishi za Afrika
- Francolinus adspersus, Kwale Domo-jekundu (Red-billed Francolin)
- Francolinus afer, Kereng'ende au Kwale Shingo-nyekundu (Red-necked Francolin)
- Francolinus africanus, Kwale Bawa-kijivu (Grey-winged Francolin)
- Francolinus ahantensis, Kwale wa Ahanta (Ahanta Francolin)
- Francolinus albogularis, Kwale Koo-jeupe (White-throated Francolin)
- Francolinus bicalcaratus, Kwale Vikwaru-viwili (Double-spurred Francolin)
- Francolinus camerunensis, Kwale wa Kameruni (Mount Cameroon Francolin)
- Francolinus capensis, Kwale Kusi (Cape Francolin)
- Francolinus castaneicollis, Kwale Kisogo-chekundu (Chestnut-naped Francolin)
- Francolinus clappertoni, Kwale wa Clapperton (Clapperton's Francolin)
- Francolinus coqui, Kwale Miguu-njano (Coqui Francolin)
- Francolinus erckelii, Kwale wa Erckel (Erckel's Francolin)
- Francolinus finschi, Kwale wa Finsch (Finsch's Francolin)
- Francolinus griseostriatus, Kwale Michirizi-kijivu (Grey-striped Francolin)
- Francolinus hartlaubi, Kwale wa Hartlaub (Hartlaub's Francolin)
- Francolinus harwoodi, Kwale wa Harwood (Harwood's Francolin)
- Francolinus hildebrandti, Kwale wa Hildebrandt (Hildebrandt's Francolin)
- Francolinus icterorhynchus, Kwale wa Heuglin (Heuglin's Francolin)
- Francolinus jacksoni, Kwale-mlima (Jackson's Francolin)
- Francolinus lathami, Kwale-msitu (Latham's Francolin)
- Francolinus leucoscepus, Kereng'ende au Kwale Shingo-njano (Yellow-necked Francolin)
- Francolinus levaillantii, Kwale Bawa-jekundu (Red-winged Francolin)
- Francolinus levaillantoides, Kwale wa Kulal (Orange River Francolin)
- Francolinus nahani, Kwale wa Nahan (Nahan's Francolin)
- Francolinus natalensis, Kwale wa Natal (Natal Francolin)
- Francolinus nobilis, Kwale Mrembo (Handsome Francolin)
- Francolinus ochropectus, Kwale wa Djibuti (Djibouti Francolin)
- Francolinus psilolaemus, Kwale-bwawa (Moorland Francolin)
- Francolinus rufopictus, Kereng'ende au Kwale Kidari-kijivu (Grey-breasted Francolin)
- Francolinus schlegelii, Kwale wa Schlegel (Schlegel's Francolin)
- Francolinus sephaena, Kwale Kishungi (Crested Francolin)
- Francolinus shelleyi, Kwale wa Shelley (Shelley's Francolin)
- Francolinus squamatus, Kwale mabaka (Scaly Francolin)
- Francolinus streptophorus, Kwale Shingo-nyeusi (Ring-necked Francolin)
- Francolinus swainsonii, Kereng'ende au Kwale wa Swainson (Swainson's Francolin)
- Francolinus swierstrai, Kwale wa Swierstra (Swierstra's Francolin)
- Xenoperdix udzungwensis, Kwale wa Udzunga (Udzungwa Partridge)
- Xenoperdix obscurata, Kwale wa Rubeho (Rubeho Forest Partridge)
[hariri] Spishi za Asia
- Francolinus francolinus (Black Francolin)
- Francolinus gularis (Swamp Francolin)
- Francolinus pictus (Painted Francolin)
- Francolinus pintadeanus (Chinese Francolin)
- Francolinus pondicerianus (Grey Francolin)