Km/h
Kutoka Wikipedia
Km/h ni kifupi cha "Kilomita kwa saa" ni kipimo cha kasi. Km pekee yake ni kifupi cha kilomita na h ni kifupi cha saa (Kilat. hora > kiing. hour).
Kitu chenye kasi ya 1 km/h kinatembea kilomita moja katika muda wa saa moja. Mwanadamu kwa mwendo wa wastani anatembea kwa 5 km/h yaani katika muda wa saa moja anatembea kilomita moja. Kwa kutumia baisikeli kwa kasi ya wastani mtu hutembea kwa 15 km/h hadi 20 km/h. Magari yanaruhusiwa kutembea kwa 50km/h mjini na 80 hadi 100 km/h nje ya miji.
Kipimo cha SI kwa kasi ni m/s yaani mita kwa sekunde lakini hakitumiki sana kwa sababu katika maisha ya kila siku watu hawataki kujua mwendo wao kwa kila sekunde.
[hariri] Viungo vya Nje
Makala hiyo kuhusu "Km/h" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Km/h kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |