Kilwa Kisiwani
Kutoka Wikipedia
Kilwa Kisiwani ni jina la kijiji kikubwa kwenye Kisiwa cha Kilwa karibu na mji wa Kilwa Masoko katika Mkoa wa Lindi, Tanzania.
Ndipo mahali pa mji wa Kilwa ya kihistoria iliyokuwa mji mkubwa kabisa kati ya miji ya Waswahili katika pwani la Afrika ya Mashariki wakati wa karne za 14. - 16. BK.
Yaliyomo |
[hariri] Mwanzo wa Kilwa walikuwa wenyeji na Washirazi
Mwanzo wa Kilwa umekadiriwa ulikuwa mnamo 800 BK. Kuna kumbukumbu ya kimdomo inayosema: Watu wa kwanza waliojenga Kilwa Kisiwani ndio Watakata, halafu watu wa Jasi wa kabila la Waranga. Badaaye akaja Mrimba na watu wake. Halafu akaja Sultan Ali bin Selimani Mshirazi yaani [[|Uajemi|Mwajemi]]. Akaja na jahazi zake akaleta bidhaa na watoto wake. Mtoto mmoja aliitwa Fatima binti Sultan Ali. Hatujui majina ya watoto wengine. Walikuja na Musa bin Amrani Albedu. (kutoka BBC: The Story of Africa - The Swahili)
[hariri] Mji muhimu zaidi wa Uswahilini
Kuanzia karne ya 11 Kilwa ilikuwa kituo muhimu ya biashara. Kuanzia karne ya 13 na 14 BK Kilwa ikawa muhimu zaidi kuliko Mombasa. Biashara yake ilikuwa dhahabu kutoka Dola la Mwene Mtapa (Zimbabwe), pembe za ndovu, chuma, nazi pamoja na kununua bidhaa kutoka Bara Hindi na Uchina. Sarafu ya dhahabu kutoka Kilwa imepatikana huko Zimbabwe Kuu.
Katika karne ya 14 -kati ya 1330 na 1340 BK- mji ulitembelewa na msafiri Mwarabu Ibn Battuta aliyeacha taarifa ya kwanza ya kimaandishi kuhusu mji.
Majengo makubwa yalijengwa ikiwa magofu yao yamesimama hadi leo kama vile msikiti kuu, nyumba ya kifalme ya Husuni Kubwa na mengi mengine.
[hariri] Kuja kwa Wareno
Kuja kwa Wareno katika Karne ya 16 ilivuruga biashara ya Waswahili. Kilwa ikarudi nyuma. Katika karne za 18. na 19. ikapata upya nguvu ya kiuchumi kutokana na biashara ya watumwa. Mwisho wa biashara hii ulimaliza utajiri wa Kilwa.
[hariri] Kilwa leo
Leo hii Kilwa Kisiwani kipo katika eneo la Tanzania lisilotembelewa kirahisi. Mawasiliano kwa barabara ni mbaya ingawa kuna majaribio ya miaka mingi kutengeneza barabara kuu kati Dar es Salaam na Lindi/Mtwara.
Hata hivyo kisiwa ni kati ya Hifadhi ya Kiutamaduni muhimu sana za Tanzania. Kilwa Kisiwani imeandikishwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" (World Heritage).