Jorge Luis Borges
Kutoka Wikipedia
Jorge Luis Borges (24 Agosti 1899 - 14 Juni 1986) alikuwa mwandishi wa fasihi kutoka nchi ya Argentina. Wataalamu wengi wa fasihi wanaamini kuwa Borges alikuwa mojawapo wa waandishi mashuhuri sana katika karne iliyopita. Borges hasa alijulikana kwa kutunga hadithi fupi za kubuniwa zilizoangazia maswala magumu kama vile "Wakati, Uwanda na Vioo" (kwa Kiingereza, Time, space and mirrors).
Mifano ya hadithi fupi alizoziandika ni kama "Shamba Panda" ambayo kwa Kiingereza ni The Garden of forking paths, na "Maktaba ya Babeli", au kwa Kiingereza, The Library of Babel.
[hariri] Viungo vya nje
- Internetaleph Jorge Luis Borges