John Eccles
Kutoka Wikipedia
John Carew Eccles (27 Januari, 1903 – 2 Mei, 1997) alikuwa mwanafiziolojia kutoka nchi ya Australia. Hasa alichunguza mawasiliano ya neva. Mwaka wa 1963, pamoja na Alan Hodgkin na Andrew Huxley alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba. Alipewa cheo cha "Sir".