Hiroshima
Kutoka Wikipedia
Hiroshima ni mji katika Japani mwenye wakazi milioni moja. Iko kwenye kisiwa cha Honshu.
Mji umekuwa maarufu duniani kwa sababu ilikuwa mji wa kwanza katika historia iliyoshambuliwa kwa bomu ya nyuklia tar. 6 Agosti 1945. Ndege ya kivita ya Marekani ikatupa bomu moja iliyoua watu 75,000 mara moja na takriban 60,000 wengine walikufa baadaye kutokana na mnururisho wa kinyuklia. Wengine waliendlea kufa kwa sababu ya kansa iliyosababishwa na mnururisho.
Mji ukajengwa upya baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Jengo la "Kuba ya Bomu ya nyuklia" ni ghofu la nyumba linalohifadhiwa kama kumbukumbu ya mlipuko. Imeingizwa katika orodha ya urithi wa dunia.