Great Barrier Reef
Kutoka Wikipedia
Great Barrier Reef ni jina la kimataifa la safu ndefu ya mwamba tumbawe inayokaa baharini mbele ya pwani la Australia kwa urefu wa kilomita 2,600.
Ni safu ya mwamba tumbawe kubwa kabisa duniani ikiwa na miamba tumbawe 2,900 ya pekee na visiwa 900 katika eneo la 344,400 km². Safu hii ya mwamba tumbawe inaonekana kutoka anga la nje upande wa mashariki-kaskazini ya Australia mbele ya pwani la Queensland.
UNEP imeiita moja kati ya maajabu saba asilia za dunia imepokelewa ktika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO..
Ni mahali muhimu kwa ekolojia ya bahari; ina aina 359 za matumbawe magumu na aina 80 za matumbawe laini, aina za sifongo 1,500 pia aina za samaki 1,500 pamoja na viumbe vingi vingine.
Great Barrier Reef inavuta watalii wengi Australia kutoka pande zote za dunia zinazovutwa na maajabu ya dunia hii chini ya maji.