Gran Canaria
Kutoka Wikipedia
Gran Canaria ni kisiwa cha Kihispania kwenye funguvisiwa ya Visiwa vya Kanari katika Atlantiki mbele ya mwabao wa Afrika ya Magharibi.
Mji mkuu pia mji mkubwa ni Las Palmas de Gran Canaria kwenye kaskazini ya kisiwa.
Uchumi wa Gran Canaria kama funguvisiwa yote ni hasa utalii. Kwenye kusini ya kisiwa kuna kitovu cha utalii kwenye sehemu za Maspalomas na Playa Inglis.
[hariri] Jiografia
Kisiwa kina umbo la duara lenye kipenyo cha 45 km na eneo la 1,560 km². Idadi ya wakazi ni mnamo 800,000.
Gran Canaria ipo kati ya visiwa vya jirani vya Tenerife na Fuerteventura kwenye 28° 0' N na 15° 35' W. Mahali pa juu ni volkeno ya Pico de las Nieves yenye kimo cha 1,949 m juu ya UB.