Filbert Bayi
Kutoka Wikipedia
Filbert Bayi (amezaliwa 23 Juni, 1953) ni mwanariadha kutoka nchi ya Tanzania aliyehudhuria Michezo ya Olimpiki mwaka wa 1980 kule Urusi upande wa mbio za umbali wa katikati na kushinda nishani ya fedha katika mbio ya mita 3000. Mwaka wa 1974 alikuwa ameboresha rekodi ya mbio za mita 1500, na mwaka wa 1975 aliboresha rekodi ya mbio za maili moja.