Chari
Kutoka Wikipedia
Mto wa Chari | |
---|---|
|
|
Mdomo | Ziwa Chad |
Nchi | Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Kamerun |
Urefu | 1,200 km |
Kimo cha chanzo | 500 - 600 m |
Mkondo | ?? |
Eneo la beseni | 669,706 km² |
Chari (Shari) ni mto mkubwa unaoishia katika Ziwa Chad. Inaanza katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ikielekea kaskazini na kuingia nchi ya Chad. Baada ya kupita mji mkuu N'Djamena mto ni mpaka na Kamerun halafu unaishia katika Ziwa Chad.
Chari inabeba 90% ya maji yote ya kuingia ziwa la Chad. Idadi kubwa ya wakazi wa nchi ya Chad wanaishi karibu na mto pamoja na mji mkuu.
Watu wanapata maisha yao mtoni kwa kilimo na uvuvi hasa samaki ya sangara.
Tawimito muhimu ni mto wa Logone, mengine ni Bahr Salamat, Bahr Sarh, Bahr Aouk na Bahr Keïta.