Barua ya pili kwa Wathesalonike
Kutoka Wikipedia
Miezi michache baada ya Mtume Paulo kuwaandikia Wakristo wachanga wa Thesalonike barua tulivu, akarudia kuwaandikia kutokana na taarifa nyingine zilizomtia tena wasiwasi.
Akawafafanulia zaidi ujio wa Bwana na dalili zake, akiwahimiza hasa kufanya kazi kwa bidii badala ya kuiacha kwa kisingizio cha kwamba, eti Kristo amesharudi (2Thes 2:1-15; 3:6-15).
Mpangilio wa barua hizo ni uleule wa barua zitakazofuata: baada ya salamu na shukrani kwa Mungu, yanafuata mafundisho ya imani, halafu maadili, na hatimaye salamu nyingine.