Barua kwa Waefeso
Kutoka Wikipedia
Barua kwa Waefeso ni kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya ambalo pamoja na Agano la Kale linaunda Biblia ya Wakristo
Mtume Paulo aliweza kuandika barua hii akiwa kifungoni Roma kati ya miaka 61 na 63 ili isomwe katika makanisa yote ya mkoa wa Asia Ndogo, wenye makao makuu Efeso.
Mafundisho yake yanalingana na yale ya barua kwa Wakolosai ila yamechimbwa zaidi, kiasi kwamba barua hii inaonekana kuwa kilele cha teolojia ya Paulo.
Pamoja na kuchambua fumbo la wokovu katika Yesu Kristo, inachambua hasa fumbo la Kanisa kama mwili wa Kristo ambamo kichwa kinaeneza wokovu ulimwenguni kote.
Kwa msingi huo inasisitiza na kudai umoja kamili kati ya waamini (Ef 1:1-2; 1:17-23; 2:11-22; 3:1-21; 4:1-16).