Anguilla
Kutoka Wikipedia
Anguilla ni kisiwa cha Antili Ndogo katika Karibi na pamoja na visiwa vidogo visivyo na wakazi ni eneo la ng'ambo la Uingereza.
Kisiwa kikubwa cha Anguilla kina urefu wa 25 km na upana wa 3 km; eneo lake ni 103 km² na idadi ya wakazi mnamo watu 13,500. Kipo upande wa mashariki ya Puerto Rico na upande wa kaskazini ya Saint-Martin.
Anguilla iliwahi kuwa sehemu ya Saint Kitts na Nevis ikajitenga 1980 na kubaki sehemu ya Uingereza wakati visiwa vingine kupata uhuru.
Jina ni neno la Kihispania kwa samaki ya mkunga kutokana na umbo lake kuwa ndefu na nyembamba.
Uchumi wa kisiwa hutegemea hasa uvuwi na utalii.
Watu wa Angulilla wana asili ya watumwa kutoka Afrika. Lugha ya ni Kiingereza.
Makala hiyo kuhusu "Anguilla" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Anguilla kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |