Albuquerque, New Mexico
Kutoka Wikipedia
Albuquerque ni mji mkubwa wa jimbo la New Mexico nchini Marekani. Kuna wakazi 484,246 (2004) na pamoja na rundiko la mji ni 712,000.
Mji uko katika eneo kati ya mto Rio Grande na milima ya Sandia.
Eneo la Albuquerque liliwahi kukaliwa na Maindio tangu mwaka 1100. Mnamo mwaka 1540 conquistador Mhispania wa kwanza Francisco Vásquez de Coronado alipita hapa mara ya kwanza akitafuta mji ya dhahabu.
Mji uliundwa na walowezi Wahispania 1706 na kupewa jina kwa heshima ya Francisco Fernández de la Cueva mtemi wa Albuquerque na mfalme mdogo wa Hispania Mpya. Pamoja na eneo lote la New Mexiko mji ulihamishwa chini ya Marekani katika karne ya 19.
Kitovu cha kihistoria bado kina majengo ya zamani ya Kihispania. Kuna pia wakazi wengi kidogo wenye asili ya Kihispania na wengine huendelea kutumua lugha ya Kihispania.