Ytri
Kutoka Wikipedia
Yttri ni elementi na metali yenye kifupi Y na namba atomia 39 katika mfumo radidia. Kiasili haipatikani kama elementi peke yake ila tu katika hali ya kampaundi na elementi mbalimbali. Baada ya kutolewa katika mchanganyiko na kusafishwa rangi yake ni nyeupe-kifedha.
Matumizi yake ni hasa kwa rangi nyekundu katika mitambo kama neli zinazoonesha rangi katika kiwamba cha televisheni au cha kompyuta.
Makala hiyo kuhusu "Ytri" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Ytri kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |