Ramadan (mwezi)
Kutoka Wikipedia
Ramadan (Kiar. رمضان) (pia: ramadhani, ramazani) ni mwezi wa tisa katika Kalenda ya Kiislamu na mwezi wa kufunga katika Uislamu.
Mwislamu mzima mwenye afya nzuri anatakiwa kufunga chakula na kinywaji machana wote.
Mwisho wa Ramadan ni sikukuu ya Idul Fitri (عيد الفطر - ʿīdu ʾl-fiṭr) ambayo ni sherehe ya furaha na kupongezana. Wailsmu hutoa zakat (zakatul-fitri زكاة الفطر) na kusali baadaye hukutana kwenye karamu.