Patagonia
Kutoka Wikipedia
Patagonia ni sehemu ya kusini kabisa ya bara la Amerika ya Kusini yenye umbo la pembetatu ndefu. Inajumlisha sehemu za kusini za Argentina na Chile. Iko kusini ya mto Río Colorado ya Argentina na mto Río Bío Bío ya Chile. Upande wa magharibi iko Pasifiki na upande wa mashariki Atlantiki zinazokutana kusini kabisa katika mlango bahari wa Magellan. Kusini ya mlango bahari iko funguvisiwa ya Tierra de Fuego (nchi ya moto).
Mikoa ya Chile ya Los Lagos, Aysen na Magallanes pamoja na mikoa ya Argentina ya Neuquén, Río Negro, Chubut, Santa Cruz na Tierra del Fuego ni yote katika Patagonia.
[hariri] Wakazi na eneo
- Wakazi = 1,740,000 (2001 census).
- Eneo = 900,000 km² pamoja na Patagonia ya Chile na Tierra del Fuego
- Msongamano wa watu = 2.21 /km²
[hariri] Jiografia
Sehemu kubwa ya Patagonia ya Argentina ni tambarare kavu kwa sababu mvua haipiti milima ya Andes. Hali ya hewa ni baridi kiasi hadi baridi.
Patagonia ya Chile inapokea mvua nyingi mlimani. Kusini penye baridi kuna barafuto kubwa.
[hariri] Uchumi
Migodi na uvuvi baharini ni muhimu. Katika nchi kavu ya kusini kuna ufugaji wa kondoo. Kaskazini kuna kilimo.