Mnara wa Eiffel
Kutoka Wikipedia
Mnara wa Eiffel (Kifaransa: Tour Eiffel) ni jengo mashuhuri la mji wa Paris nchini Ufaransa. Mnara huu ulijengwa kando ya mto Seine 1887 hadi 1889 kama geti ya Maonyesho ya Dunia ya 1889. Kimo chake ni mita 300 na juu yake kuna antena ya redio jumla ya kimo inafikia mita 324. Kati ya 1889–1930 ilikuwa jengo kubwa la dunia.
Mnara huu ulipokea jina lake kutoka kwa mjenzi wake aliyekuwa mhandisi Alexandre Gustave Eiffel. Kila mwaka hutembelewa na wageni milioni sita wanaoipanda kwa kutumia ngazi 1,665.
Mwanzoni watu wa Paris hawakupenda mnara wengine walidai ubomolewe mara moja baada ya maonyesho. Lakini idadi kubwa ya watalii iliufanya kuwa ishara ya mji wa Paris na watu walianza kuuzoea. Mwaka 1906 mnara uliwezesha mawasiliano ya kwanza kwa simu hewa kati ya Ulaya na Marekani kuvukia Atlantiki kwa sababu ya kimo chake kikubwa. Wanajeshi walikuwa na kituo cha mawasiliano ya simu mnarani.
[hariri] Viungo vya Nje
muluzi arrested