Jumapili
Kutoka Wikipedia
Jumapili ni siku ya kwanza katika juma (wiki) ya siku saba yenye asili ya kiyahudi-kikristo. Iko kati ya siku za Jumamosi na Jumatatu. Kwa Wakristo wengi ni siku ya sala za pamoja kanisani.
Yaliyomo |
[hariri] Kiswahili, Kiarabu na utamaduni wa Kiislamu
Katika lugha ya Kiswahili jina la siku lina namba "2" ndani yake. Hii ni dokezo la asili ya Kiswahili katika utamaduni ya Kiislamu pasipo na athira ya Uyahudi unaoanza hesabu baada ya sikukuu ya Kiislamu ya Ijumaa siku ya sala ya pamoja: Jumamosi kama siku ya kwanza baada ya Ijumaa, Jumapili kama siku ya pili, Jumatatu kama siku ya tatu n.k.. Tabia hii katika Kiswahili ni ya pekee hasa kwa sababu Kiarabu ambacho ni lugha ya Korani takatifu na lugha ya kimataifa ya Waislamu kinafuata hesabu ya Kiyahudi na kuiita siku "al-ahad" yaani "ya kwanza".
[hariri] Siku ya jua, siku ya Bwana, siku ya ufufuo
Katika lugha za Kigermanik siku hii ina jina la "jua". Lugha hizi kama Kiingereza au Kijerumani zinaendeleza urithi wa Roma ya Kale na zaidi wa Babiloni ambako kila siku ya wiki ilikuwa chini ya mungu fulani aliyeonekana kama nyota.
Kundi lingine la lugha linatumia lugha "siku ya Bwana" yaani "Bwana Yesu Kristo". Ni hasa lugha za Kirumi kama Kifaransa (dimanche), Kiitalia (domenica), Kihispania (domingo) na kadhalika.
Lugha ya Kirusi inaita siku hii "voskresenye" yaani siku ya ufufuo.
[hariri] Uzoefu wa Kikristo
Wakristo wa madhehebu mengi isipokuwa Wasabato wanatazama Jumapili kama siku ya mapumziko iliyochukua nafasi ya Sabato iliyotajwa kwenye Amri Kumi za Agano la Kale. Sababu ya badiliko ni ufufuo wa Kristo unaokumbukwa kwenye siku ya kwanza kufuatana na habari za Agano Jipya.
[hariri] Jumapili katika lugha mbalimbali
Lugha | Jina/Matamshi | Maana | Maelezo |
---|---|---|---|
Kiebrania | יום ראשון jom rishon |
siku ya mwanzo | |
Kigiriki | Κυριακή kiriaki |
(siku ya) Bwana | |
Kiarabu | أحد al-ahad |
(siku) ya kwanza | |
Kiajemi | :یکشنبه yek-schanbe |
(siku ya) kwanza | |
Kireno | Domingo |
(siku ya) Bwana | |
Kilatini | dies solis | Siku ya jua | |
Kiitalia | domenica | (siku ya) Bwana | |
Kihispania | Domingo | (siku ya) Bwana | |
Kifaransa | dimanche | (siku ya) Bwana | |
Kijerumani | Sonntag | siku ya jua | |
Kiingereza | Sunday | siku ya jua |
Siku za juma (wiki) |
---|
Jumapili - Jumatatu - Jumanne - Jumatano - Alhamisi - Ijumaa - Jumamosi |