Frits Zernike
Kutoka Wikipedia
Frits Zernike (16 Julai, 1888 – 10 Machi, 1966) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uholanzi. Hasa anajulikana kwa uvumbuzi wake wa hadubini iwezeshayo kuangalia vyembe hai. Mwaka wa 1953 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.