Beta
Kutoka Wikipedia
Beta (Kigiriki: Βήτα, Β/β) ni herufi ya pili katika alfabeti ya Kigiriki. Ilikuwa pia na maana ya alama kwa namba 2.
Katika Kigiriki cha kale ilitaja sauti ya "B". Katika Kigiriki cha kisasa imekuwa alama ya sauti "V".
Jinsi ilivyo kawaida na herufi mbalimbali za kigiriki inatumiwa kama kifupi kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hesabu na fizikia. Imejulikana hasa kama jina la pembe ya pili katika pembetatu.
Katika falaki inatumiwa sana kwa hesabu ya nyota katika kundinyota. Kwa mfano nyota yetu jirani katika ulimwengu inaitwa "Alfa Centauri". Imeitwa hivyo kwa sababu inang'aa kushinda nyota zota za kundinyota ya Centaurus. Inayofuata ni "beta Centauri" na kadhalika.
Katika programu za komyuta "toleo la beta" (=beta-version) humaanisha toleo la awali la programu. Wahariri wanaitoa kama imeshakamilika lakini kabla ya kuiuza wanatoa nakala kwa majaribio ili makosa yaonekana.