Kundinyota
Kutoka Wikipedia
Kundinyota ni idadi ya nyota zinazoonekana angani kuwa kama kundi la pamoja.
Tangu zamani watu walitazama nyota kama nukta na kuwaza kuwa na mistari kati yao hivyo kuona picha. Kundinyota zinazojulikana sana ni kama vile Orion, Skorpio (nge), Andromeda, Msalaba wa Kusini.
Kujumlisha nyota hivi ilikuwa msaada kwa watu kukumbuka na kutambua nyota.
Hali halisi nyota hizi zinaonekana tu kama kundi lakini haziko mahali pamoja angani kwa sababu zinaweza kuwa mbali sana kutoka nyota nyingine inayoonekana kama sehemu ya kundinyota ileile.
Lakini hadi leo kundinyota 88 zinazokubaliwa ni msaada wa kukuta nyota angani.
[hariri] Mfano wa Orion
Picha za Orion katika makala hii zinaonyesha njia kutoka nyota angani hadi wazo la kundinyota. 1. Orion inaonekana vizuri kwa sababu kuna kwanza nyota tatu kama mstari. Juu yake upande wa kushoto kidogo ni nyota mbili zinazong'aa sana. Chini ya mstari wa nyota tatu kuna nyota mbili au tatu (inategemea ubora wa macho) za karibu sana. Halafu chini yake kuna tena nyota mbili za mbali kidogo zinazong'aa na kufanana zile mbili za juu. Kama giza inaongezeka ni tena nyota zaidi zinazoonekana.
2. Watu waliunganisha nyota kwa kuwaza mistari wakaanza kumwona mtu. Nyota tatu za katikati(δ, ε, ζ) ziliitwa ukanda, nyota mbili za kung'aa za juu (α, λ) zikawa mabega ya mtu na nyota mbili za chini (β,κ) miguu yake. Nyota mbili au tatu chini ya "ukanda" (ι, θ) zikatajwa kama silaha inayoaliki kwenye ukanda. Nyota nyingine hafifu zaidi zikaunganishwa katika picha hii: nyota za "π" 1,2,3 zikawa ama ngao au kando la nguo; λ kama kichwa.
3. Wasanii walichora picha kama ile ya juu upande wa kushoto (nyota kadhaa zilitiwa rangi katika makala hii kwa kuonekana vizuri zaidi si picha yenyewe). Hivyo katika mawazo ya watu wa kale katika tamaduni mbalimbali anga lilijaa mapepo au hasa miungu.
[hariri] Kundinyota na utabiri wa unajimu
Kundinyota zimekuwa muhimu kwa ajili ya unajimu. Ni hasa kundinyota 12 za Zodiaki zinadaiwa umuhimu wa kutawala tabia za watu.
Hata kama falaki imeshatambua ya kwamba kundinyota hazipo ni wazo tu tukitazama kutoka kwetu duniani; hali halisi angani hazipatikani badu unajimu inatangaza tofauti.