Aswan
Kutoka Wikipedia
Aswan (أسوان, Aswān pia Assuan au Assouan) ni mji wa kusini kabisa nchini Misri mwenye wakazi 200,000. Ni makao makuu ya mkoa wa Aswan. Imejulikana duniani kutokana na lambo la Aswan ambalo ni ukuta mkubwa unaozuia mwendo wa mto Nile na kusababisha kutokea kwa bwawa la Nasser.
Tangu kutengenezwa kwa lambo Aswan imekuwa mji wa viwanda kwa sababu umeme unapatikana kwa wingi tangu 1960.
Utalii ni muhimu pia kwa sababu karibu na Aswan kuna mabaki mengi ya mahekalu na majengo mengine ya enzi za Misri ya Kale.
[hariri] Historia
Zamani mji ulijulikana kwa jina la Syene au Swan au Seveneh. Inatajwa katika Biblia. Ilikuwa mji muhimu wa Misri ya kusini na mara nyingi mpaka na madola ya Sudan. Hivyo Mafarao waliweka hapa kituo muhimi cha kijeshi kwa karne nyingi.
Aswan ilikuwa muhimu katika historia ya sayansi. Wazee walitambua ya kwamba wakati wa mchana jua iko juu kabisa angani na fimbo halina kivuli katika saa ya mchana. Mtaalamu Mmisri Eratosthenes alianza hapa upimaji wake uliothebitisha ya kuwa dunia si tambarare lakini duara kama mpira.