Adolf Butenandt
Kutoka Wikipedia
Adolf Friedrich Johann Butenandt (24 Machi, 1903 – 18 Januari, 1995) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa alichunguza homoni zisababishazo kuvutiwa kijinsia. Mwaka wa 1939, pamoja na Leopold Ruzicka alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia. Serikali ya Ujerumani walimlazimisha kukataa tuzo lakini aliruhusiwa kuipokea mwaka wa 1949.