Walter Brattain
Kutoka Wikipedia
Walter Houser Brattain (10 Februari, 1902 – 13 Oktoba, 1987) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza uhandisi wa umeme na kuvumbua transista. Mwaka wa 1956, pamoja na William Shockley na John Bardeen alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.