Stevie Wonder
Kutoka Wikipedia
Stevie Wonder |
|
---|---|
|
|
Jina la Kiraia | Steveland Hardaway Judkins |
Jina la kisanii | Steve Wonder |
Nchi | Marekani |
Alizaliwa | 13 Mei, 1950 |
Aina ya muziki | R&B soul funk Motown |
Kazi yake | Mwimbaji Mtunzi Mwanaala Mtayarishaji |
Miaka ya kazi | 1961–hadi leo |
Ala | Sauti Vyombo tofauti |
Kampuni | Motown |
Stevie Wonder (amezaliwa tar. 13 Mei, 1950 mjini Saginaw, Michigan). Jina lake halisi ni Steveland Hardaway Judkins lakini alibadili jina lake la mwisho na kuliweka jina la ndoa la mamake, Morris.
Ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji, mwanamuziki na mwanaharakati wa haki za binaadam wa Kimarekani. Amekuwa kipofu tangu kuzaliwa kwake. Wonder amekuwa miongoni mwa wasanii waliowakubwa na wenye mafanikio-kujulikana katika studio ya kurekodia ya Motown.
Amerekodi zaidi ya albamu 23 na kutoa vibao vingi vilivyo maarufu kabisa. Alitunga na kuzirekodi mwenye baadhi ya nyimbo zake na za watu wengine vilevile. Wonder vilevile ni mpigaji wa ngoma, gitaa, sinthesaiza, congas, na pia almaarufu kwa kupiga kinanda na harmonica.