Sega
Kutoka Wikipedia
Sega ni nafasi ambako nyuki hutunza asali. Ina vyumba vingi vidogo vyenye umbo la pembesita. Nyuki hutengeneza sega kwa nta.
Yaliyomo |
[hariri] Kazi ya sega
Sega huwa na kazi mbili:
- ni chumba cha kulea jana za nyuki yaani mayai ya nyuki hutegwa humo na nyuki changa zinakua ndani yake.
- mahali pa kutunza akiba ya asali
Vyumba vya jana vinatengenezwa tofauti kwa sababu kuna aina tatu za nyuki katika kila mzinga wenye ukubwa tofauti:
- vyumba vya wafanyakazi vya kawaida huwa na urefu wa milimita 10-12
- vyumba vya dume walio wachache huwa na urefu wa 14 mm
- vyumba vya malkia atakayetega mayai na kuwa mama wa wote huwa na urefu wa 20-25 mm na kujengwa kando la sega.
[hariri] Sega za Nyigu
Nyigu ambao ni wadudu karibu na nyuki hutengeneza pia aina ya sega lakini wanajenga kwa karatasi. Wachache wao hutunza pia asali.
[hariri] Sega katika ufugaji wa nyuki
Katika ufugaji nyuki wa kisasa mzinga wa nyuki huwa na fremu ndani ambamo nyuki zinajenga sega. Fremu ya sega zinatolewa moja-moja bila kuharibu mzinga. Baada ya kuondoa asali fremu inarudishwa ilhali vyumba vya sega bado viko na nyuki zinaanza upya kujaza vyumba bila kupoteza muda wa kujenga sega mpya. Faida yake -kama ntaa haihitajiwi- ni kuongeza mavuno ya asali. Nyuki hutumia takriban kilogramu nane za asali kutengeneza kilogramu moja ya nta ama kwa njia ya kula asali au kwa njia ya kutotengeneza asali kwa kaziy a nta.
Katika ufugaji nyuki wa kienyeji mzinga wa nyuki hubomolewa wakati wa kutoa sega. Sega hizi hazilingani kwa umbo na ukubwa hazirudishwa tena.
[hariri] Matumizi
Nta ya sega ina matumizi yake kwa kutengeneza mishumaa au sabuni. Katika nchi kadhaa asali huuzwa ndani ya sega. Wafuga nyuki hula sega yote.
Makala hiyo kuhusu "Sega" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Sega kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |