Polykarp Kusch
Kutoka Wikipedia
Polykarp Kusch (26 Januari, 1911 – 20 Machi, 1993) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza sifa za kisumaku za elektroni. Mwaka wa 1955, pamoja na Willis Lamb alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.