Peter Jackson
Kutoka Wikipedia
Peter Jackson |
|
---|---|
|
|
Jina la kuzaliwa | Peter Jackson |
Alizaliwa | 31 Oktoba, 1961 New Zealand |
Kazi yake | Mwongozaji Mwandaaji Mwandikaji wa script |
Ndoa | Fran Walsh (1987-) |
Peter Jackson (amezaliwa tar. 31 Oktoba, 1961, mjini Pukerua Bay) ni mwongozaji filamu wa Kinew Zealand. Anafahamika zaidi kwa kuongoza mfululizo wa filamu ya The Lord of the Rings.
Mnamo mwaka wa 2003, Jackson alishinda tuzo ya Academy kwa kuongoza filamu ya The Lord of the Rings: The Return of the King. Vilevile anafahamika kwa kuitengeneza upya filamu ya King Kong ya mwaka 2005. Jackson alizaliwa katika mji wa Pukerua Bay, New Zealand, na ni mtoto pekee wa mzee Bill na Joan Jackson, ambao wote walikuwa wahamiaji kutoka nchi ya Uingereza.
[hariri] Filamu alizoongoza
- Bad Taste (1987)
- Meet the Feebles (1989)
- Valley of the Stereos (1992) (filamu fupi)
- Braindead (a.k.a. Dead Alive) (1992)
- Heavenly Creatures (1994)
- Forgotten Silver (1995) - mockumentari
- The Frighteners (1996)
- The Lord of the Rings: The Fellowship of the Ring (2001)
- The Lord of the Rings: The Two Towers (2002)
- The Lord of the Rings: The Return of the King (2003)
- King Kong (2005)
- The Lovely Bones (2007) (Ishatangazwa)
- Halo (2008) - Mwandaaji mkuu (Ishatangazwa)