Kigujarati
Kutoka Wikipedia
Gujarati (ગુજરાતી gujǎrātī?) ni lugha muhimu nchini Uhindi.
Kinajadiliwa na watu milioni 46 duniani. Ni kati ya lugha rasmi 22 za shirikisho la Uhindi na lugha rasmi ya jimbo la Gujarat katika Uhindi ya magharibi.
Wasemaji wa Kigujarati zaidi ya milioni 45 huishi Uhindi na wengi wao wako kwenye jimbo la Gujarat. Takriban 400,000 hukadiriwa katika Afrika ya Mashariki ni lakhi mbili na nusu Tanzania na lakhi moja na nusu Kenya. Uingereza wako karibu lakhi tatu na mnamo lakhi moja huko Pakistan.
Kinahesabiwa kuwa kati ya lugha za Kihindi-Kiajemi ndani ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Lugha za karibu ni pamoja na Urdu, Kihindi, Kipunjabi, Kisindhi, Kimarathi na Kibengali.
Asili ya kutokea kwa Kigujarati ilikuwa Kisanskrit iliyokuwa lugha ya chanzo cha utamaduni wa Uhindi.. Kigujarati cha Kale kilipatikana kama lugha ya fasihi tangu mnamo mwaka 1100.
Kigujarati huandikwa kwa mwandiko wake wa pekee ambao ni abugida inayofanana na Devanagari ya Kihindi.
Mfano:
કેમ છો? (kem cho?) Habari zako? (salamu ya kawaida)