Johannesburg
Kutoka Wikipedia
Johannesburg (inayojulikana pia kama iGoli) ni jiji kubwa katika nchi ya Afrika Kusini. Ni mji mkuu wa jimbo la Gauteng.
Mji ulianzishwa 4 Oktoba 1886 ukakua haraka baada ya kupatikana kwa dhahabu. Siku hizi ni kitovu cha kiuchumi wa Afrika Kusini na makao ya soko la hisa kubwa katika Afrika.
Hata kama ni mji mkubwa haiko kati ya miji mikuu mitatu ya Afrika Kusini lakini mahakama ya katiba inakaa hapa.
Nyumba kubwa ya maofisi katika Afrika yote ni jengo la Carlton Centre lenye maghorofa 50 kuna pia jengo la juu kabisa ambalo ni Hillbrow Tower (mita 270 au maghorofa 90).
Karibu theluthi moja ya wakazi wa jiji hukaa katika eneo la Soweto ambalo ni mtaa ulioengwa nje ya jiji asilia kwa ajili ya wafanyakazi Waafrika wakati wa Apartheid (siasa ya ubaguzi wa rangi).