Hukwe Zawose
Kutoka Wikipedia
Hukwe Zawose huyu alikuwa ni mwanamuziki wa kiasili wa kitanzania, na muziki wake hasa ulikuwa ni wa kabila la Wagogo. Kipaji chake cha muziki kiligunduliwa na aliyekuwa rais wa kwanza wa Tanzania hayati J. K. Nyerere wakati alipofanya ziara mkoa wa Dodoma. Alivutiwa na muziki wa Hukwe, na aliporudi Daressalaam alimuita Hukwe kwenye kikundi cha utamaduni cha Taifa.