Herbert Spencer Gasser
Kutoka Wikipedia
Herbert Spencer Gasser (5 Julai, 1888 – 11 Mei, 1963) alikuwa mwanafiziolojia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza na kugundua kazi za neva mwilini. Mwaka wa 1944, pamoja na Joseph Erlanger alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.