Gambia (mto)
Kutoka Wikipedia
Mto wa Gambia | |
---|---|
|
|
Chanzo | Nyanda za juu za Futa Djalon, Guinea |
Mdomo | Atlantiki kwa mji wa Banjul |
Nchi | Guinea, Senegal & Gambia |
Urefu | 1,120 km |
Kimo cha chanzo | 900 m takriban |
Mkondo | hadi 2000 m³/s kutegemeana na majira na kiasi cha mvua njiani |
Eneo la beseni | 69,931 hadi 87,850 km² (maelezo hutofautiana) |
Gambia ni mto inayoanza katika milima ya Futa Djalon huko Guinea. Inafuata njia ya kunyoka hadi Atlantiki. Mdomo wake ni pana sana.
Baada ya kutoka katika Futa Djallon mto unaelekea kaskazini-magharibi kupitia mkoa wa Tambakunda katika Senegal halafu mbuga wa wanyama wa Niokolo Koba. Hapa inapokea tawimiti ya Nieri Ko and Kuluntu na kuingia katika nchi ya Gambia karibu na mji wa Fatoto.
Kuanzia hapa mto unaelekea magharibi tu isipokuwa kwa njia ya kunyokanyoka. Takriban 100 km kabla ya kufika mdomo unaanza kupanuka ukiwa na upana wa 10 km mdomoni mwenyewe.
Mto una visiwa mbalimbali ndani yake, vikubwa zaidi ni kisiwa cha Tembo na kisiwa cha MacCarthy. Kisiwa cha James Island mdomoni kabisa ilikuwa kituo muhimu cha biashara ya watumwa imeandikishwa katika orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia.
Kutokana na upana na uwingi wa maji Gambia inafaa kama njia ya maji; meli za baharini zinaingia takriban 280 km ndani.
Miji mikubwa zaidi mtoni ni Basse Santa Su, Janjanbureh na Banjul.
[hariri] Viungo vya nje
en: The Gambia Basin